Majaliwa ameyasema hayo wakati akiwasalimia wazee wa Dar es salaam katika mkutano wa wazee hao na Rais John Magufuli ambapo amesema kuwa hawatawaangusha watanzania kwani lego lao ni kuhakikisha nchi inazidi kusonga mbele.
''Tunaomba mtuunge mkono kwa dhati tutafanya kazi kwa malengo na manufaa ya watanzania na hakika hatutawaangusha''
Aidha kwa upande wa Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu amesema kwamba wananchi waamini kwamba serikali itatenda kwa vitendo na wanaodhani kuwa ni kazi wanazofanya kuwa ni nguvu za soda watambue kuwa kazi hiyo itaendelea kwa manufaa ya watanzania.






