Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa.
Akiongea na Wananchi katika viwanja vya stand mwanuzi Wilayani Meatu,Mkoani Simiyu, Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa, amesema kuwa wananchi wengi wanalalamika kunyanyaswa na wawekezaji wakubwa hivyo amezitaka mamlaka husika kuchukua hatua juu ya migogoro hiyo.
Waziri Mkuu Majaliwa amesema Serikali haiweze kutoa dhamana na kuwavumuliwa wanaojiita wawekezaji na kisha kufanya mambo ya hovyo hivyo amamemtaka mkuu wa Mkao wa Simiyu kufuatilia malalamiko ya wananchi juu ya mwekezaji wa pori la akiba la makao.
Kauli hiyo imekuja baada ya Mbunge wa Jimbo la Meatu Salum Khamis, kutoa kilio cha wananchi ambao wamekua wakilalamika kunyanyaswa na muwekezaji huyo na kusema kuwa hilo ni jipu ambalo linapaswa kutumbuliwa ili kuwapa ahueni wananchi hao.