Waziri ofisi ya Rais Tamisemi Mhe.George Simbachawene
Waziri ofisi ya Rais Tamisemi Mheshimiwa George Simbachawene amesema kwasasa hakuna halmashauri hata moja nchini ambayo inauwezo wa kujitegema kwa asilimia 10 yamatumizi yake yakibajeti iliyojitengea , hivyo kusababisba Serikali kuwa na mzigo mkubwa wa bajeti.
Waziri Simbachawene ameyasema hayo kwenye mahojiano maalum kuhusu namna serikali ilivyoboresha njia zaukusanyaji wa kodi, hata hivyo ameelekeza kuwa ni lazima halmashauri na idara zake zihakikishe zinakusanya mapato yake kwa lengo lakusaidia jamii na kuendesha shughuli zake za kila siku.
Amesema vitu vinavyochangia ukosefu wa mapato ni pamoja na uzembe ambao unafanywa na wakuu wa idara mbalimbali kuanzia serikali za mitaa.
Waziri Simbachawene amesema katika kupambana na upotevu wa fedha za uma, ofisi yake imeweka taratibu kwa kila idara kuanzia Serikali za mitaa kukusanya mapato yake kwa njia yakieletroniki ili kuhakikisha kodi za wananchi zinarudi kuleta maendeleo kwa ujumla.
Ameongeza katika kuhakikisha kodi wanazotozwa wananchi haziwaumizi(kodi za kero)wameweka na kuainisha utaratibu maalum wa shughuli ambazo zinapaswa kulipiwa kodi hivyo kuwataka viongozi kaacha kuwasumbua watanzania wa hali ya chini kwakua Serikali inafidia pesa hizo.
Kuhusu utaratibu wakukusanya kodi kwa njia ya kieletroniki amesema tayari halmashauri zaidi ya 90 zimeunganishwa na mfumo huo na kama mfumo huo ukitumika bila kuchakachuliwa basi Serikali inategemea kuongeza pato lake la Taifa.
Aidha amezishauri halmashauri kukusanya mapato yaliyowekwa kisheria na sio kuwaumiza wanyonge na pesa hizo wahakikishe zinaboresha maisha ya watanzania bila kujali itikadi zao kwakua Serikali niya watanzania wote.





