
Naibu Waziri wa Uvuvi na Mifugo Saning’o Ole Telele akiteta jambo na mkulima.
Akiongea katika kilele cha maadhimisho ya siku ya uvuvi duniani iliyofanyika kitaifa mkoani Kagera Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Saning’o Ole Telele amesema Tanzania imejaliwa kuwa na rasilimali nyingi ikiwemo Mito, Maziwa, Bahari na Mabwawa na kwamba ili kufanikiwa kupitia rasilimali hizo ni wajibu wa watanzania kulinda na kuziheshimu rasilimali hizo kwa kuvua samaki kwa kufuata sheria na kanuni za uvuvi zilipo hapa nchini.
Naye Katibu Mkuu wa Wizara yaMaendeleo ya Mifugo na Uvuvi Yohana Budeba na Afisa Uvuvi Mkoa wa Kagera ametoa wito kwa watanzania kujikita zaidi kwenye ufugaji wa samaki hatua ambayo itasaidia kuwainua watanzania.
Kwa upande wake Aporinali Kyojo wamesema pamoja na kuhudhuria maadhimisho hayo wametembelea baadhi ya wananchi wanaojihusisha na ufugaji wa samaki ambapo amesema sasa ni wakati wa wavuvi kuweza kuinua uchumi wa Taifa kutokana na ufugaji.