
Kamanda Muroto ametoa taarifa hiyo jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo alieleza kijana Mazengo Chati mwenye umri wa miaka 28, amembaka mama yake mzazi mwenye miaka 56 na ametenda kosa hilo kwa madai ya ulevi pamoja na imani za kishirikina.
Kamanda Muroto amesema kuwa "tukio la kijana Mazengo limetokea katika Kijiji cha Manchali ambapo kijana huyo alimlawiti mama yake mzazi akiwa hajitambui, na kwa sasa tunamshikilia kwa ajili ya kumfikishwa mahakamani"
Aidha Kamanda huyo amesema kuwa Jeshi la Polisi mkoani Dodoma linawashikilia watu wengine wawili, kwa makosa ya ulawiti na ubakaji wa watoto na wazee huku mtuhumiwa mmoja akiuawa na wananchi wenye hasira kali, baada ya kukutwa akiwa anambaka mwanafunzi wa miaka nane.