Thursday , 7th Apr , 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amezitaka nchini wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kushirikiana kwa ukaribu ili kujiletea maendeleo ya kweli.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe

Rais Dkt. Magufuli amesema hayo jana wakati wa uzinduzi rasmi wa daraja la kimataifa na kituo cha kutoa huduma kwa pamoja mpakani katika eneo la Rusomo lililoko mpaka mwa Tanzania na Rwanda.

Rais Magufuli amesisitiza umoja na mshikamano wa nchi wanachama wa Umoja huo ikiwa ni pamoja na kufanya biashara pamoja kunaweza kuleta maendeleo ya kweli kwa wananchi wanachama wa Jumuiya hiyo.

Rais Magufuli amezitaja nchi hizo wanachama ikiwemo Tanzania, Uganda, Kenya, Rwanda, Burundi pamoja na iliyoingizwa siku hizi ya Sudani ya kusini ambapo inafanya kuwa na jumla ya watu milioni 165 kama wakishamana katika biashara basi maendeleo yataonekana.

Sauti ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongelea nchi wanachama kushirikiana.