Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akibeba taka katika zoezi la Usafi wa mazingira uliofanyika jana
Uzinduzi huo wa sherehe za mapinduzi ya kutimiza miaka 52 ulifanyika kwa zoezi la Usafi wa mazingira nchi nzima ambapo Dkt. Shein aliongoza wananchi na askari wa vikosi vya ulinzi na Usalama kushiriki zoezi hilo katika soko la Mbogamboga lilipo Mombasa wilayani Magharibi.
Akiongea mara baada ya Usafi huo Dkt. Shein amesema kuwa Wanzabzibar wanapaswa kujivunia mapinduzi yaliyofanyika mwaka 1964 kwa kuwa yameleta faida kubwa na mabadiliko makubwa kwa jamii.
Akizungumzia suala la usafi kwa nchini nzima Dkt. Shein ameendelea kuwalaumu wahusika wa kuweka nchi katika mazingira ambapo amesema sheria zipo lakini wahusika wamekua ni wazito kuchukua maamuzi na kufanya zoezi hilo kuwa gumu.
Miradi 18 inatarajiwa kuzunduliwa na mawe nane ya masingi yanatarajiwa kuwekwa na viongozi mbalimbali katika sherehe hizo hadi kufikia kilele cha maadhimisho ya siku hiyo hapo januari 12 ambapo rais Dkt. Shein anatarajia kulihutubia taifa.