Dkt Chamuriho ametoa kauli hiyo leo alipokuwa akifungua kongamano lililowakutanisha wadau wa ujenzi kujadili namna ambavyo wanaweza kumaliza tatizo la rushwa kwenye sekta hiyo na kuongeza kuwa ni lazima kuwepo na uwazi katika matumizi ya maendeleo ya fedha za ujenzi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mpango wa uwazi katika sekta ya ujenzi CoST Mhandisi Kazungu Magili amesema kuwa ni muhimu kuzingatia sheria kwani sheria zenyewe zinasisitiza kuwa na uwazi lakini watendaji wanashindwa kuzifuata.