Moja ya viwanda vinavyotumia teknolojia ya FESTO.
Teknolojia hiyo imeingizwa nchini kwa ushirikiano baina ya taasisi inayoongoza duniani kwa mitambo ya kisasa ya uzalishaji viwandani ya FESTO yenye makao makuu yake nchini Ujerumani na Tume ya Sayansi na Teknolojia - Costech itakayoanza kufundishwa katika Chuo cha Teknolojia cha jijini Dar es Salaam – DIT.
Akizungumza mara baada ya kutembelea maabara tatu zilizopo katika chuo cha DIT na ambazo ndiyo zitatumika kufundishia wanafunzi pamoja na wafanyakazi wa viwandani; Katibu Mkuu wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Patrick Makungu amesema uwepo wa maabara hizo kutasaidia kupunguza idadi ya wanafunzi wanaokwenda nje ya nchi kusomea uhandisi wa fani za kisasa viwandani.
Kwa upande wake, Katibu mkuu wizara ya mawasiliano, sayansi na teknolojia, mhandisi Profesa Patrick Makungu amesema kuwa idadi kubwa ya vijana wa kitanzania wanaokwenda nchi za nje kwa ajili ya kujifunza fani na mbinu mbalimbali za kisasa kwa maswala ya maendeleo hasa ya kimitandao sasa itaanza kupungua baada ya kujengwa kwa maabara hizo.
Mhandisi Makungu amesisitiza kuwa vijana wanatakiwa waanze kutumia fursa hiyo kujiajiri wenyewe kutokana na ujuzi watakaoupata kupitia maabaara hizo za kisasa na bora katika taasisi hiyo.
kwa upande wake mkuu wa chuo hicho Prof. John Kondoro amesema kuwa vifaa hivyo vikitumika vizuri na walimu na wanafunzi serikali na nchi kwa ujumla inategemea mabadiliko makubwa ya kimaendeleo.