Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mh.Mwigulu Nchemba amesema mtu anapofanya tukio la kinyama au kigaidi akamatwe mhusika aliyefanya hilo tukio nasio kuhusisha tukio hilo la kigaidi na dini yake,kitendo cha kumhusisha jambazi au gaidi na imani yake ya dini kunahatarisha umoja wetu.
Mheshimiwa Mwigulu ameyasema hayo kwenye kongamano la viongozi wa dini mbalimbali kutoka pande zote za nchi Tanzania Bara na Visiwani,kongamano lililokua linajadili kuhusu matukio ya Ugaidi nchini na duniani kote.
Kwa upande wa serikali Mwigulu amesema wanaendelea kuchukua hatua za kupambana na matukio ya kinyama na yanayoashilia ugaidi na kuwataka viongozi wote wa dini wa ngazi zote kuendelea kufanya kazi kwa pamoja kuanzia ngazi ya juu hadi chini kabisa ili kuhimarisha usimamizi wa usalama wa raia,makazi na nyumba zetu za ibada.
Viongozi walioshiriki kongamano hilo ni pamoja na Mufti mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakary Zubeir, Askofu mkuu wa KKKT Mchungaji Alex Malasusa.




