Sunday , 2nd Oct , 2016

Mkuu wa wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe Andrea Tsere, amewaweka ndani Meneja na Mwenyekiti wa bodi ya Saccos ya Mlangali na kuivunja Bodi yake na kutoa siku 30 kwa Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa Upotevu wa milioni 114

Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Andrea Tsere akiwa katika kijiji Mbugani kata ya Mavanga wilayani humo

Mkuu huyo wa Wilaya pia ameagiza wanachama wa Saccos hiyo kulipa deni la marehemu ambaye alikuwa meneja wa awali aliyefariki kwa kujinyonga mwaka 2012.

Maamuzi hayo yanakuja baada ya kuwepo kwa sintofahamu ya matumizi ya fedha za wanachama na fedha nyingine kulipa hasara iliyosababishwa na marehemu.

Mwenyekiti wa muda wa Saccos hiyo Nasanael Mgani anasema kuwa katiba ya Saccos hiyo ilikiukwa na uongozi wa marehemu na wa sasa kwa kuwa katiba ya chama hicho haikutumika.

Wanachama wa chama hicho wanasema kuwa uamuzi ulio chukuliwa utasaidia kurejeshwa kwa fedha zao.

ANDEA TSERE, MKUU WA WILAYA LUDEWA
UONGOZI 1. NASANASEL MGANI, MWENYEKITI WA MUDA 2. FREDERICK NZIKU, KATIBU WA MUDA
WANACHAMA 1. ADREA MWINUKA, MWANACHAMA 2. JAMES NGEHA, MWANACHAMA 3. SESILIA SANYIKA, MWANACHAMA