Friday , 15th Jan , 2016

Serikali imeiagiza watendaji wa wakala wa mabasi yaendayo haraka (DART), kufanyia kazi changamto zilizopo ikiwamo suala la nauli iliyopendekezwa ili kutumiwa katika kipindi cha mpito.

Naibu Wazri ,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI),Suleiman Jaffo

Akizungumza na watendaji wa Dart Naibu Wazri, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Suleiman Jaffo aliyefanya ziara ya kujifunza shughuli zinazofanywa na Dart amesema hatua iliyofikia ya awamu ya kwanza ni nzuri.

Mhe. Jaffo amesema kwa sasa wananchi wanategemea kuona mradi huo ukianza kufanya kazi ili kuwapunguzia adha ya usafiri lakini suala la nauli iliyopendekezwa na mtoa huduma huyo limekuwa kero kubwa kwao.

Jaffo ameongeza kuwa nauli hizo zilizopendekezwa na mtoa huduma hazikubaliki na kutaka Dart kusimamia nauli zilizopo katika mkataba na ndizo zinazopaswa kujadiliwa ili kuwatendea haki wananchi.