Friday , 18th Dec , 2015

Chama cha Walimu Tanzania (CWT) mkoani Mtwara kimeendesha mafunzo ya siku tatu kwa viongozi wa chama hicho kutoka katika ngazi ya mkoa, wilaya na vitengo vya wanawake, kwa lengo la kuwajengea uwezo juu ya masuala mbalimbali yakiuongozi.

Baadhi ya walimu wa Mkoa wa Mtwara wakiwa katika Moja ya Semina.

Mafunzo hayo yaliyoratibiwa na baraza kuu la CWT Taifa na kuhusisha viongozi kutoka katika wilaya zote za mkoa wa Mtwara, ndio yakwanza tangu kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa chama hicho mwezi Mei mwaka huu.

Wakizungumza baada ya kufungwa kwa mafunzo hayo, baadhi ya walimu wamesema awali walikuwa wakikabiliwa na changamoto nyingi za kiuongozi zaidi ikiwa ni juu ya matumizi ya fedha za chama ambazo walishindwa kupangilia mlolongo mzuri.

Katibu wa chama hicho, Fratten Kwahison, amesema kupitia mafunzo haoyo, walimu wameweza kupata ufumbuzi wa mambo mbalimbali ambayo yalikuwa ni kikwazo kwao katika utendaji wa kazi zao pamoja na mifumo dume ambayo ilikuwa ni changamoto kwa walimu wakike.