Wednesday , 23rd Sep , 2015

Mgombea urais kupitia Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharrif Hamad amewaahidi Wazanzibari endapo atapata ridhaa kuwa rais ,serikali yake itaunda sheria mpya ya rushwa ili kupambana na wala rushwa kwa nguvu zote.

Mgombea urais kupitia Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharrif Hamad

Maalim Seif ambaye pia ni makamu wa kwanza wa rais wa Zanzibar ametoa ahadi hiyo huko Chaani mkoa wa Kaskazini Unguja katika mkutano wa kampeni za urais alipokuwa akiwahutubia wananchi ambapo amemesema serikali yake itapigania suala rushwa kwa nguvo zote na kuifikisha Zanzibar katika kiwango cha asilimia sifuri.

Akizungmzia utendaji wa serikali Maalim Seif amesema serikali yake ambayo itafuata ilani ya CUF, itawapiga marufuku wakuu wa mikoa,Wilaya na mashekha kufanya au kujingiza katika shughuli za siasa na kazi zao zitakuwa ni za kuwatumikia wannchi pekee.

Haraakati hizo za kampeni za urais kisiwani Zanzibar zinarajiwa kusimama kwa siku nne ili kupisha waislamu hapa nchini na dunaini kusheherekea sikuu ya Eid El Haj ambapo Zanzibar kawaida sikuu kama hizo sherehe zake huwa kwa siku nne huku baadhi ya vyama vya siasa vikiwa havijanonekana kabisa katika kunadi wagombea wake.