
Tukio hilo la ukombozi lilitokea tarehe 26 mwezi wa kwanza mwaka 1986.
Harakati hizo ziliongozwa na Yoweri Kaguta Museveni kupitia chama cha NRM – (National Resistance Movement).
Harakati za ukombozi zilianza baada ya uchaguzi wa Desemba 10 mwaka 1980, uchaguzi uliokuwa na upinzani wa hali ya juu.
Awali Yoweri Museveni ambaye muanzilishi wa Uganda Patriotic Movemend alikusanya baadhi ya wanaharakati waliokuwa na mlengo kama wake na kuanza mazoezi ya vita vya msituni.
Baadaye, kundi la Museveni likaungana na wapigania uhuru wengine na kuunda chama cha NRA (National Resistance Movement).
Wakati harakati za NRM zinaendelea, pia kulikuwa na makundi mengine ya waasi yaliyokuwa yakipigania ukombozi, kama vile UNRF (Uganda National Rescue Front).
Mnamo mwezi Julai 27, 1985, mapinduzi ya kijeshi yalitokea yakiongozwa na Luteni Jenerali Bazilio Olara-Okello.
Okero
Mapinduzi hayo hayakuwafurahisha waasi, hivyo mazungumzo ya amani yalisitishwa na kusababisha vita, ambayo haikudumu kwa muda mrefu. Na mnamo tarehe 25 Januari 1986 NRA walifanikiwa kuikomboa Uganda kutoka katika serikali ya kijeshi.
Na mnamo tarehe 29 Januari, 1986, Yoweri Museven aliapishwa na kuwa Rais wa Uganda, na ameendelea kuwa Rais wan chi hiyo hadi leo ambapo amewangoza wananchi wa taifa hilo kuadhimisha miaka 31 ya Ukombozi.
Eatv limited tunawatakia waganda wote sherehe njema za kukumbuka mapinduzi ya uganda
Hizi ni baadhi ya nukuu zilizowahi kutolewa na Rais Museveni kwa nyakati tofauti
1
“NO ONE SHOULD THINK THAT WHAT IS HAPPENING TODAY IS A MERE CHANGE OF GUARD; IT IS A FUNDAMENTAL CHANGE IN THE POLITICS OF OUR COUNTRY.”
“Mtu yoyote asifikirie haya yaliyotokea ni mabadiliko tu ya ulinzi, ni msingi wa mabadiliko katika siasa za nchi yetu”
Museveni
2
THE PROBLEM OF AFRICA IN GENERAL, AND UGANDA IN PARTICULAR IS NOT THE PEOPLE BUT LEADERS WHO WANT TO OVERSTAY IN POWER
“Tatizo la Afrika kwa ujumla; na Uganda kipekee siyo watu bali viongozi wanaotaka kung’ang’ania madarakani”
3
I WAS AGAINST IMPUNITY WHEN IT COMES TO HUMAN RIGHTS VIOLATIONS, BUT MANY OF US AFRICAN LEADERS NOW WANT TO LEAVE THE ROME STATUTE AS SOON AS POSSIBLE BECAUSE OF THIS WESTERN ARROGANCE
“Nilikuwa kinyume na ukatili lilipokuja swala la ukiukwaji wa haki za binadamu. Lakini hivi sasa, wengi wetu sisi viongozi wa Kiafrika tunataka kuacha amri za kiroma haraka iwezekanavyo kwasababu ya kiburi cha magharibi”