Friday , 7th Aug , 2015

Aliyekuwa mwanaseheria mkuu wa serikali na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge ameendelea kuliburuza Baraza la Sekretarieti ya Maadili kwa kutumia vifungu mbalimbali vya sheria

Aliyekuwa mwanaseheria mkuu wa serikali na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge ameendelea kuliburuza Baraza la Sekretarieti ya Maadili kwa kutumia vifungu mbalimbali vya sheria ya maadili ya viongozi wa umma na kuwataka mawakili wake kuisoma sheria vizuri.

Katika mfululizo wa maswali aliyoulizwa Chenge kwa siku ya pili leo ameendelea kushikilia msimamo wake wa kutokuwepo kwa muingiliano wa maslahi kwa kudai kuwa amepewa fedha kutoka kampuni ya VIP Enginieering and Marketing kulingana na kazi aliyokuwa anaifanya.

Katika mahojiano hayo kati ya Chenge na baraza hilo yalichukua zaidi ya saa moja ambapo baada ya kumalizika, Mwenyekiti wa baraza hili Jaji Hamis Msumi aliairisha usikilizwaji wa shauri hilo hadi pale mlalamikiwa atakapowasilisha majibu dhidi ya hati ya malalamiko atakayowasilishiwa kutoka kwenye baraza hilo.

Akijibu swali la wakili wa baraza hilo Hassani Mayunga lililomtaka kueleza kama aliingiza taarifa za malipo yake kutoka VIP Chenge amesema hakuona haja ya kuingiza kwenye matamko yake kwanin haikuwa sehemu ya malipo ya mkataba wake ulivyohitajika.

Chenge alisema wakati Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakati ikiingia mkataba na IPTL hakuishauri Serikali akiwa kama Chenge bali Ofisi ya Mwanasheria ndio iliyomshauri.

"Mimi sikuishauri Serikali bali ni Ofisi ya Mwanasheria Mkuu kwani ni taasisi na inajukumu la kuishauri Serikali sio mimi kama Chenge," alisema.