Sunday , 24th May , 2015

Kamati kuu ya Chama Cha Mapinduzi imeishauri serikali kushauriana na tume ya Taifa ya Uchaguzi ili kwa pamoja waweze kutafuta njia muafaka ya kulihitimisha na kulishughulikia suala la kura ya maoni na kulitatua kwa maslahi mapana ya Taifa.

Katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na Wanahabari akifafanua kuhusiana na ripoti na maazimio ya kikao cha kamati kuu cha CCM.

Hayo yamesemwa leo na Katibu wa Itikadi na uenezi wa CCM, Nape Nnauye wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma kuhusiana na ajenda mbalimbali zinazojadiliwa na kamati kuu ya CCM.

Nape amesema kuwa hiyo imetokana na changamoto mbalimbali zilizoonyweshwa katika mchakato wa maandalizi ya kura hiyo na kuzingatia hali halisi ya mchakato huo na kutafuta njia muafaka ya kulishughulikia na kulihitimisha suala hilo kwa maslahi ya Taifa.

Nape amezitaka kati ya changamto zinazolikabili zoezi hilo ni pamoja na changamot inayolikumba zoezi la uandikishaji wa Dafati la kudumu la Mpiga kura ambapo mpaka sasa linakwenda kwa kusuasua.

Aidha ameongeza kuwa Sheria ya kura ya maoni ni changmoto nyingine kwa kuwa siku 60 za kutoa elimu na siku 30 za kampeni ambazo ukitazama na muda uliobaki kwa ajili ya uchaguzi mkuu ni jambo ambalo litaifanya kura hiyo kutofanyika.

Pia Nape amesema kuwa na muda uliopo katika kuufika uchaguzi mkuu pamoja na maadalizi yake ni changamto nyingine inayolikabili zoezi hillo la kura ya maoni kwa kuwa cuhaguzi mkuu ni lazima katika tarehe iliyopangwa.

Nape amesema serikali na tume ni lazima wakae ili kufanya uamuzi wa Busara na kulitatua suala hilo kwa maslahi ya taifa.