Wednesday , 14th Nov , 2018

Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa, Phillip Mangula amewapokea madiwani watatu wilayani mvomero ambao wamehama kutoka vyama vya upinzani na kujiunga na na Chama Cha Mapinduzi CCM kwa sababu ya kumuunga mkono Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Chama Cha Mapinduzi.

Katika Wilaya hiyo ya Mvomero jumla ya madiwani wawili wa CHADEMA akiwemo Lucas Mwakambaya wa kata ya Mtibwa na Timotheo Machoka wa kata ya Chenzema pamoja na Adam Msimbe kata ya Mangae Kupitia Chama Cha Wananchi CUF.

Akizungumza mbele ya madiwani hao Makamu huyo Mwenyekiti wa CCM taifa amesema kwa sasa chama hicho kimefunga mjadala wa kuwapokea wapinzani wanaohamia chama hicho kufuatia chaguzi ndogo za marudio kutumia fedha nyingi.

Kupitia Kamati kuu Maalum ya Halmashauri kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi CCM, kilitangaza novemba 15 kuwa ndiyo mwisho wa Chama hicho kuwapokea wabunge na madiwani ambao wamekuwa wakitangaza nia ya kujiunga na Chama hicho na kupewa tena nafasi ya kugombea.

Uchaguzi wa marudio umesusiwa na vyama vya upinzani nchini kwa kile walichokisema kutokuwepo kwa uwanja sawa uchaguzi pamoja na kubariki kile walichokidai ni kubariki matumizi mabaya ya fed