Monday , 1st Jun , 2015

Mbunge wa bunge la Afrika Mashariki mh Charles Makongoro Nyerere, hatimaye ametangaza nia yake ya kugombea urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia chama cha mapinduzi CCM.

Makongoro Nyerere akivalishwa vazi la mgolole kama ishara ya kupewa baraka za wazee katika mbio zake za urais

Katika tukio hilo lililofanyika leo katika eneo la Mwitongo mita chache tu toka kaburi la baba wa taifa wilayani Butiama mkoani Mara makongoro amekataa kuzungumzia kabisa ajenda zake za mipango ya maendeleo kwa Tanzania hivi sasa kwa maelezo kuwa chama hicho kina taratibu zake kwa kufuata ilani ya CCM inayotarajia kupitishwa mapema mwezi Julai mwaka huu.

Amesema inasikitisha kuona baadhi ya mawaziri na viongozi ccm ambao wamejitokeza kugombea nafasi hiyo lakini wameanza kuishutumu serikali yao kwa kutaja vipaumbele vyao kabla CCM haijatoa ilani yake.

Aidha mh Makongoro ametumia nafasi hiyo kuwalaumu baadhi ya viongozi wakuu wa serikali kutumia nafasi zao serikalini hivi sasa kuwatisha wakurugenzi wa majiji, manispaa na halmashauri za wilaya kwa kutaka kupewa fedha za kuwawezesha kugombea nafasi ya urais huku wakifikia hatua ya kufukuza wakurugenzi kazi wanaoshindwa kutii maagizo hayo.

kuhusu tatizo la rushwa nchini, mtoto huyo wa tano wa baba wa taifa hayati mwl Julius Kambarage Nyerere,amesema CCM imekithiri kwa rushwa na kusababisha tatizo ambalo limesambaa kwa taifa zima hata kuwanyima haki baadhi ya watu na kusabisha chama hicho kuwa na makundi makubwa yanayotishia amani hivyo kuomba ridhaa hiyo kwa wana CCM ni katika kurejesha chama hicho kwa wanachama.

Awali wazee wa kijiji cha Butiama wakiongozwa na chief wa kabila la wamemvisha nguo aina mgolole na kukabidhi fimbo ikiwa ni sehemu ya kumpa baraka za kugombea nafasi hiyo.