Friday , 9th Jan , 2015

Mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali CAG Profesa Mussa Asaad  amesema ofisi yake itaendelea kufanya kazi  kwa kuzingatia vigezo weledi na maadili  ili kujenga heshima ndani na nje ya nchi.

Mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali CAG Profesa Mussa Asaad

CAG pia amewataka  watumishi wa ofisi  za ukaguzi kote nchini  kutambua wajibu wao  kufanya kazi   ya ukaguzi inayokidhi viwango vya kimataifa.

Profesa Asaad ameyasema hayo mjini Morogoro wakati wa hafla fupi ya kumkaribisha  iliyoandaliwa  na ofisi ya mdibiti na mkuaguzi mkuu hesabu za serikali,  ambapo  amesema ukaguzi ni muhimu kwa maendeleo ya taifa.

Ameongeza kuwa, kuna umuhimu wa kuweka utaratibu wa  kuwajengea uwezo watumishi  wa ofisi hiyo mara kwa mara ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao.

Katibu mkuu kiongozi Ombeni Sefue  ameziagiza  wizara idara na taasisi za serikali kuzingatia utekelezaji na ushauri unaotolewa na ofisi ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa serikali  akisema ushauri huo sio wa hiari ni wa lazima  na zaidi wanahitaji kujipanga  kudhibiti matumzi mabaya ya fedha za umma  kwani   wanaoiba rasilimali za taifa nao wamebaini mbinu  mpya.