Tuesday , 24th Mar , 2015

DAFTARI la kudumu la wapiga kura kwa mfumo wa BVR katika halmashauri ya Njombe, limeendelea vizuri huku walio tumika katika kata za awali kutumika katika kata wanazo zianza leo na kesho katika halmashauri hizo.

Waandikishaji wakiwa wanasubiri wananchi kujiandikisha Mjini Njombe.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Kituo hiki mkoani Njombe maofisa uchaguzi wasaidisi wa halmashauri za mkoani hapa wamesema kuwa watawatumia waandikishaji waliowatumia katika kata walizo anza nazo ili kuhakikisha changamoto za utumiaji wa mashine kuto jitokeza.

Ofisa uchaguzi msaidizi wa halmashauri ya Makete Gregory Emmanuel amesema kuwa katika halmashauri yake wamefanikiwa kuandikisha watu wengi kupita makadilio yao na kufikia asilimia 139 ambapo walitarajia kuwaandikisha watu 10859 na kuwaandikishwa watu 15142.

Kwa upandewake Ofisa uchaguzi msaidizi wa halmashauri ya Ludewa, Gervas Lupembe amesema kuwa katika halmashauri yake wamefanikiwa kumaliza kata 6 kati ya kata 25 za halmashauri hiyo na kuwa kata moja jana wangeimalizia kutokana na kata hiyo kuanza kwa kuchelewa kutokana na vifaa kufika kwa kuchelewa.

Amesema kuwa katika kata zake sita walizo anzanazo na kuwa hakuna kata waliyoongeza muda kutokana na watu kujitokeza kwa wakati na kumaliza siku ya juzi ambayo zilikuwa zinatimia siku saba.

Naye afisa uchaguzi halmashauri ya Wanging’ombe, Christopher Mashaka amesema kuwa katika kata zao walizo anzanazo nne wamefanikiwa kuwaandikishwa watu wote na kuwa waendelea na kata 5 na kuwatumia waandikishaji walewale walio anzania na kuwa wataongeza wachache kutoka 108 na kuwa 114 ili zoezi hilo kwenda vizuri.

Amesema kuwa wanaimani kuwa zoezi hilo kwa halmashauri hiyo wanauhakika kwenda viruri kwa kuwa wamejipanga kuzifanyia marekebisho mashine ili kutokumbana na mashine kukwamakwama na kuwa changamoto za mwanzo huenda sisijitokeze.

Aidha kwa halmashauri ya Njombe Mjini Ofisa uchaguzi msaidizi Swigha Sanke, amesema zoezi hilo limeendelea vizuri na kuwa kwa siku ya jana ndio wanamalizia kwa vituo vilivyo kuwa vina watu wengi na kubakia, ambapo waliwaandika majina na kumalizia hiyo jana

Kwa halmashauri ya wilaya NjombeOfisa uchaguzi msaidizi, Dominick Manyenyi amesema kuwa katika halmashauri hiyo zoezi limeendelea vizuri licha ya baadhi ya kata kuanza kwa kuchelewa kutokana na kuwapo kwa changamoto za miundombinu na kuwa kwa kata zinazo fuata watajitahidi siku ya Leo kuhakikisha mashine zinafika kwaajili ya kuaza huku siku ya jana wakifanya usafirishaji na marekebisho.