Wednesday , 30th Nov , 2016

Mkurugenzi wa Shirika la Ujasusi nchini Marekani CIA John Brennan amemuonya Rais mteule wa nchi hiyo Donald Trump kwamba ikiwa atasitisha mkataba wa nyuklia na Iran litakuwa jambo la hatari na la kustaajabisha.

John Brennan

Katka mahojiano aliyofanya na shirika la utangazaji la Uingereza  BBC, John Brennan amemshauri Rais mpya kuihofia Urusi na ahadui zake na kuilaumu nchi hiyo kwa mateso makubwa ya binadamu nchini Syria.

Wakati wa Kampeni za urais nchini Marekani Trump alitishia kufuta makubaliano ya Nukilia yaliyofikiwa kati ya Marekani na Iran na kugusia kufanya kazi kwa karibu na Urusi.

Brennan atajiuzulu nafasi hiyo mwezi Januari baada ya kulitumikia shirika hilo kwa miaka minne.

Donald Trump