Kamishna wa Ardhi nchini Tanzania, Bw. Moses Kusiluka amesema zoezi la kubomoa nyumba lililofanyika jana Kurasini eneo la Shimo la Udongo Jijini Dar es Salaam limefanyika kwa kuzingatia sheria zote na haki.
Bw. Kusiluka ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema serikali tayari imekwishahakiki na kutoa malipo ya fidia kwa wale wanaobomolewa nyumba zao na kuahidi kuendelea na uchunguzi wa kubaini watendaji wanaokula fedha za fidia.
Aidha Kusiluka meongeza kuwa kuongeza kuwa kwa upande wa serikali tayari imeshahakiki na kutoa malipo ya fidia kwa wale wanaobomolewa nyumba zao nakuahidi kuendelea na uchunguzi wao wakuwabaini watendaji wanakula hela za fidia zinazotakiwa kupelekwa kwa watanzania wanaobomolewa kwaajili ya kupisha ujenzi maalum.