Baadhi ya bidhaa za Chakula zinazotumika kupika Futari katika mwezi mtukufu wa Ramadhani
Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Dkt. Rehema Nchimbi amewataka wafanyabishara kutopandisha bei za bidhaa mbalimbali wakati huu wa msimu wa Mwezi mtukufu wa Ramadhani ili kuzipata Baraka za mwezi huu.
Wakulima wamedaiwa kupandisha bei za bidhaa za mazao kipindi hiki cha Ramadhani katika mkoa huo na kusababisha bei kuwa juu ya bidhaa zinazotumika katika msimu huu wa funga ya ramadhani.
Wakizungumza na East Africa Radio mkoani Dodoma Baadhi ya wafanyabishara wanao nunua bidhaa kutoka kwa mkulima ikiwa ni pamoja na Abubakari Athuman wa soko la Majengo amesema kuwa wao wakifika kwa wakulima wanakuta bei zipo juu kuliko walivyo kuwa wakitarajia hivyo kusababisha wao kupandisha bei za bidhaa.