
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla
Dkt. Kigwangala ametoa ahadi hiyo akiwa katika moja ya mikutano yake katika jimbo la Nzega Vijijini ambapo amesema amechukua maamuzi hayo ikiwa ni kutoa sadaka kwa tukio lililomtokea.
Matokeo ya ajali ile ingeweza kuwa mbaya zaidi kuliko haya niliyoyapata, sina la ziada bali ni kumshukuru mungu kwa kutoa sadaka ya kuwasomesha watoto 5 zaidi pale Nzega mjini pamoja na kusomesha watoto wasiojiweza katika jimbo la Nzega Vijijini''. Amesema Kigwangalla
Aidha Kigwangalla amesema “nitawakatia bima ya afya wakina mama na wazee ili wawe na uhakika wakupata huduma ya afya, nimeshaanza mchakato wa kuwatambua watu wenye uhitaji na hivi karibuni nitatoa msaada wangu.”
Agosti 4 mwaka huu Waziri Dkt. Hamisi Kigwangalla alipata ajali mbaya ya barabarani katika kijiji cha Magugu Mkoani Manyara baada ya gari lake alilokuwa akisafiria kupinduka na kupelekea kifo cha aliyekuwa Afisa Habari wake Hamza Temba.