Friday , 3rd Mar , 2017

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema jumla 11,503 watuhumiwa wa uzalishaji, usambazaji, uuzaji na utumiaji wa dawa za kulevya wamekamatwa kwa kipindi cha Julai mwaka jana hadi Januari mwaka huu nchini.

Waziri Mkuu akiongoza kikao cha Baraza la Mawaziri

Akizungumza leo katika kikao cha Baraza la Mawaziri cha kwanza tangu Serikali kuhamia mjini Dodoma, Majaliwa amesema katika kipindi hicho kesi za kujibu zilikuwa ni 9,811 ambapo watuhumiwa 941 walikutwa na kesi za kujibu huku 238 wakiachiwa huru na kesi 478 bado zinaendelea mahakamani.

Kuhusu pombe za viroba, Majaliwa  amesema oparesheni inaendelea katika mikoa mbalimbali baada ya kupigwa marufuku Machi Mosi mwaka huu na kwamba kupitia oparesheni hiyo wamegundua mambo mengine ikiwemo uwepo wa makampuni yaliyokuwa hayalipi kodi.

Kwa upande wa ajenda za kikao hicho cha mawaziri, Majaliwa amesema wizara zitatoa takwimu za watumishi wangapi waliohamia, idadi ya watumishi wote,  wamepanga awamu ngapi za kuhamia Dodoma kati.

Msikilize hapa....