Wednesday , 12th Nov , 2014

Watanzania wana fursa kubwa ya kutumia mazao ya asali yanayopatikana kwa wingi hapa nchini kukuza vipato vyao na kuboresha afya zao.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda.

Akizungumza baada ya kuwatembelea maonyesho ya wazalishaji wa asali wanaoshiriki kongamano la kimataifa la Ufugaji wa Nyuki Barani Afrika linalofanyika Arusha Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda amesema licha ya mazao ya asali kuwa tiba ya maradhi mbalimbali soko hilo ni kubwa na linaendelea kukua kutokana na kuongezeka kwa watu wanaotumia asali zaidi kuliko sukari.

Mh. Pinda amesema kuwa Serikali kwa sasa wapo katika mpango wa kuwezesha makabala mbalimbali ambayo Chanzo chao kikubwa cha mapato na chakula ni asali lakini pia kutoa elimu kwa vijana mbalimbali na makundi tofauti juu ya ufugaji wa nyuki na faida zake.

Baadhi ya wadau akiwemo Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu wameelezea hatua zinazochukuliwa kukuza soko la mazao ya misitu ikiwemo asali huku baadhi ya waashriki washriki wakieleza changamoto mbalimbali zinazowakabili.