Thursday , 19th Nov , 2015

MTOTO wa miaka 16 mkazi wa kijiji cha Mbwila wilayani Ludewa mkoani Njombe Simon Dastani amefariki dinia baada ya kupigwa kwa fimbo na kaka yake baada ya kukutwa akifanya mapenzi na Nguruwe mali ya mkazi wa kijiji hicho.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe Wilbroad Mtafungwa

MTOTO wa miaka 16 mkazi wa kijiji cha Mbwila wilayani Ludewa mkoani Njombe Simon Dastani amefariki dinia baada ya kupigwa kwa fimbo na kaka yake baada ya kukutwa akifanya mapenzi na Nguruwe mali ya mkazi wa kijiji hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Wilbroad Mtafungwa alisema kuwa kijana huyo aliuawa baada ya kaka yake kusikia kijana huyo ameidhalilisha familia yao kwa kufanya mapenzi na mnyama na kuanza kumchapa fimbo kitu kilicho sababisha kutoka damu nyingi na kupelekea kifo chake.

Alisema kuwa katika tukio hilo kaka wa marehemu, Sylvester Dastani alikimbia baada ya kuona hali ya ndogo wake kuwa mbaya na kuwa jeshi la polkisi mkoani Njombe kwa kushirikiana na wananchi wanamtafuta kijana huyo ili kumtia hatiani.

Alisema kuwa kaka huyo aliamua kuchukua hatua ya kumpiga na fimbo ndogo wake baada ya kuona ameizalilisha familia yao na baada ya kumchapa na fimbo alimfunga na kamba kijana huyo.