Amber Ruty
Aidha kesi hiyo itaanza kusikilizwa maelezo ya awali Machi 7, mwaka huu. Awali kesi hiyo ilipangwa kutajwa mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustine Rwizile.
Hata hivyo, Wakili wa Serikali Faraja Nguka alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na kuomba tarehe ya kuwasomea washtakiwa maelezo ya awali.
Hakimu Rwizile amesema washtakiwa watasomewa maelezo hayo Machi 7, mwaka huu na dhamana yao inaendelea ambapo amewataja washtakiwa wengine ni pamoja na Saidi Mtopali na James Charles Maarufu kama James Delicious.
Katika kesi ya msingi, ilidaiwa kuwa washtakiwa walifanya mapenzi kinyume na maumbile ambalo linamkabili Amber Ruty, inadaiwa alitenda kosa hilo kati ya ama baada ya Oktoba 25, 2018 ambapo alimruhusu Said Mtopali kumuingilia kinyume na maumbile, huku akijua ni kosa kisheria.