Thursday , 15th Oct , 2015

Amani na usalama kwa wanawake ndiyo chachu ya maendeleo kwa kundi hilo amesema Naibu waziri wa maendeleo ya jamii jinsia na watoto wa Tanzania Pindi Chana wakati akilihutibia baraza la usalama la Umoja wa Mataifa ambalo limejadili azimio namba 1325.

Naibu Waziri wa maendeleo ya jamii jinsia na watoto Mh. Pindi Chana

Mh. Chana amesema licha ya changamoto kadhaa zinazokabili nchi ikiwamo mila potofu na sheria kandamizi, hatua za kuhakikisha amani na ustawi kwa wanawake zimepigwa katika ustawi wa wanawake kwa kuzingatia amani na maendeleo.

Aidha naibu waziri huyo amesisitiza zaidi Tanzania inapoelekea kwenye uchaguzi mkuu muhimu ni vyama vikaweka sera madhubiti za kuwalinda wanawake na watoto ili kuleta maendelo endelevu.

Amesema kuanzishwa kwa dawati la jinsia katika kila kituo cha polisi ili kukabiliana na ukatili dhidi ya wanawake kumeleta mabadiliko makubwa.