Monday , 4th Jan , 2016

Watu wawili wamefariki na wengine 21 kujeruhiwa baada ya basi la abiria la Luwinzo lililokuwa likitokea Njombe kwenda Dar es Salaam kugonga lori, katika eneo la Mafinga, wilayani Mufindi mkoani Iringa.

Ajali ya basi la luwinzo na roli iliyotokea leo eneo la Mafinga wilayani Mufindi Mkoani Iringa

Akiongea na East Africa Radio Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa ACP Ramadhan Mungi amesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa basi lililotaka ku over-take lori hilo lakini kukawa na gari nyingine mbele jambo lililopelekea dereva kuepusha basi lake kugongana uso kwa uso na badala yake kuliparamia lori hilo.

Kamanda Mungi amesema watu waliofariki katika ajali hiyo wote ni Watumishi wa gari hilo Mmoja akiwa ni Kondakta na mwengine ni msimamizi na kuongeza kuwa mpaka wanawashikilia maderva wa magari yote mawili kwa ajili ya Uchunguzi Zaidi.