Monday , 14th Sep , 2015

Wahisani kutoka shirika la AGRA wameahidi kuendelea kusaidia serikali ya Tanzania katika miradi zaidi ya utafiti,ikiwemo kuelekeza nguvu zake kwenye maonesho ya umuhimu wa viazi lishe vilivyofanyiwa utafiti na kituo cha utafiti cha naliendele kilicho

Mratibu wa utafiti wa zao la Muhogo na jamii ya viazi kitaifa,kutoka taasisi ya utafiti ya Naliendele,Dkt. Geoffrey Mkamilo,

Mwakilishi wa AGRA katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika Dkt. George Bigirwa, amesema hayo baada ya kuwatembelea wananchi wakiwemo waliokumbwa na mafuriko wanaoishi kwenye mahema katika kambi maalum ya mateteni,iliyopo kata ya Magole wilayani Kilosa mkoani Morogoro, ambao walinufaika na mbegu za viazi lishe vyenye vitamini A kwa wingi ikilinganishwa na viazi vya kawaida.

Aidha ameahidi wataiwezesha zaidi Taasisi ya Naliendele kufanya maonesho ya wazi ili wananchi wengi waone umuhimu wa kuzalisha na kutumia viazi hivyo ambavyo mbali na sifa ya kuzaa kwa wingi,vinahimili ukame ikilinganishwa na mazao mengine.

Kwa upande wake mratibu wa utafiti wa zao la muhogo na jamii ya viazi kitaifa, kutoka taasisi ya utafiti ya Naliendele, Dkt. Geoffrey Mkamilo, amesema walilenga kusambaza mbegu hizo za viazi lishe kwa wakulima wa wilaya za Gairo na Kilosa kutoka na maeneo hayo kuathiriwa zaidi na ukame na kwamba viazi ni zao lao kubwa na tegemeo la biashara.