Monday , 13th Jun , 2016

Chama cha ACT – Wazalendo kimeelezwa kusikitishwa kwake na kitendo cha jeshi la polisi cha kuweka ulinzi mkali na kukizuia chama hicho kufanya kongamano lake

Chama cha ACT – Wazalendo kimeelezwa kusikitishwa kwake na kitendo cha jeshi la polisi cha  kuweka ulinzi mkali na kukizuia chama hicho kufanya kongamano lake katika jengo la Millenium Tower jijini Dar es salaam jana mchana .
 
Akiongea na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa ACT – Wazalendo, Mama Anna Mghwira amesema,  kitendo hicho  ni kuminya demokrasia na kuongeza kwamba, juhudi za kupambana na ufisadi nchini haziwezi kufanikiwa endapo ukandamizaji wa demokrasia utaendelea..

Kadhalika Mama Mghwira anesena, kongamano hilo lililenga kumpa fursa Mbunge wa Kigoma Mjini kupitia chama hicho, Mh. Zitto Kabwe, kusema yale ambayo angeongea Bungeni hasa baada ya yeye na Wabunge wenzake sita kusimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge la Bajeti.