Monday , 6th Jun , 2016

Chama cha ACT – Wazalendo kimekosoa uongozi wa Rais Dk. John Mgufuli kwa kile ilichokielezea kwamba, anataka kujenga utawala wa kiimla.

Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Kabwe Zitto akihutubia

Kauli hiyo imetolewa jana jijini Dar es salaam na kiongozi wa chama hicho ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Mjini, Mh. Zitto Kabwe, wakati wa uzinduzi wa “Operesheni Linda Demokrasia” katika viwanja vya Mbagala Zakheem.

Mh. Zitto amesema, Rais anapaswa kuwa na utu na wananchi wake, asikilize kwanza na kuchambua mambo kabla ya kusema chochote mbele ya hadhara.

Ameongeza kuwa, chama cha ACT – Wazalendo kinamuunga mkono Rais kutokomeza ufisadi lakini kinampinga kwa kutokomeza demokrasia yenye misingi madhubuti ya uwajibikaji ambalo ndio jawabu sahihi dhidi ya ufisadi na unyonyaji nchini.

Sauti ya Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Kabwe Zitto akihutubia