Wyre aota mafanikio makubwa
Wyre, msanii wa muziki kutoka Kenya ameweka wazi ndoto zake kubwa za kuongeza wigo wa soko la muziki wa reggae kutoka Afrika Mashariki katika ngazi ya kimataifa, lengo lake kubwa likiwa ni kuona wasanii kutoka ukanda huu wakiwa wanashiriki katika matamasha makubwa ya Kimataifa.