Emeka amtishia mwenye nyumba wake
Mwigizaji maarufu wa filamu wa nchini Nigeria Emeka Ike, ametishia kufungua kesi ya madai ya fidia ya Naira bilioni 2 zaidi ya shilingi bilioni 19 za Tanzania kutoka kwa mwenye nyumba wake, kwa ajili ya usumbufu na hasara aliyoipata katika kesi ya madai ya kodi inayoendelea dhidi yao kwa sasa.