Chameleone anyang'angwa gari na URA
Muda mchache kabla ya kuanza kwa onyesho kubwa la Tubonge la msanii Jose Chameleone huko Uganda, msanii huyu alijikuta akipata chngamoto kutoka kwa mamlaka ya mapato ya nchini Uganda URA, ambao wameweka gari yake aina ya escallade kizuizini kwa madai ya kiasi kikubwa cha kodi ambacho wanamdai msanii huyu.
Tukio hili liliingilia ratiba ya mazoezi ya msanii huyu muda mchache kabla ya onyesho lake lililofanyika kwa mafanikio makubwa, ambapo baada ya mabishano ya hapa na pale, msanii huyu alikubali kuwaachia gari hilo mpaka pale watakapofikia suluhu ya jambo hili.