Ngorongoro Heroes wajigamba kuifunga Kenya
Kocha wa timu ya taifa ya vijana walio na umri chini ya miaka 20 Ngorongoro Heroes John Simkoko amesema kikosi chake kiko imara tayari kupambana na Kenya katika mechi ya marudiano ya mchujo kuwania kushiriki fainali za mataifa ya Afrika kwa vijana.