JK ajivunia kazi iliyofanywa na vikosi vya usalama
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ameviaga vikosi vya usalama nchini huku akijivunia ufanyaji wao kazi na kuiweka nchi salama pamoja na raia wake licha ya changamto wanazokumbana nazo.
