ACT-Wazalendo kuwanufaisha wananchi na Rasilimali
Mgombea Urais wa Tanzania kupitia chama cha ACT-Wazalendo, Anna Mngwira, amesema iwapo chama hicho kitapata ridhaa ya kuongoza nchi, kitahakikisha rasilimali za madini, gesi asilia na mafuta zinamilikiwa na wananchi kikatiba.