Samatta aingia tatu bora Tuzo Mchezaji Bora Afrika
Mshambulizi matata wa Taifa Stars ya Tanzania na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Mbwana Samatta ametajwa katika orodha ya wachezaji watatu bora na shirikisho la soka la Afrika CAF wanaocheza soka barani Afrika.

