'Mama ntilie' waomba kuwezeshwa waachane na kuni
Wafanyabiashara wa vyakula vya kupika maarufu kama mama ntilie, wameliomba Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, kuwapatia majiko ya gesi ili waweze kuandaa vyakula na kufanya biashara zao katika mazingira nadhifu.