Tutakula sahani moja na waamuzi - Bodi ya Ligi
Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB) imesema miongoni mwa mambo itakayoyaangalia kwa umakini mkubwa katika mzunguko wa pili wa ligi ni waamuzi, ili kuhakikisha wanatenda haki na kuondoa malalamiko yaliyoshamiri katika mzunguko wa kwanza.

