Wafanyakazi waigomea serikali
Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) limepinga kanuni mpya ya kukokotoa mafao ya wastaafu iliyotolewa hivi karibuni likisema inakandamiza wafanyakazi na kusema pendekezo lao lilikuwa ni kuunganishwa kwa mifuko ya hifadhi ya jamii na si kanuni mpya ya vikokotoo inayolalamikiwa.