Upelelezi wa aliyemchoma moto mke wake wakamilika
Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon, ameileza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa, upelelezi wa kesi ya mfanyabishara Khamis Saidy, anayekabiliwa na mashtaka ya mauaji baada ya kumuua na kisha kumchoma moto mke wake Naomi Marijani, tayari umekwishakamilika.