Waziri afafanua kuhusu kupanda kwa bei ya Sukari
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa amewatoa hofu Watanzania kutokana na kupanda kwa bei ya sukari na kusema nchi imeagiza tani zaidi ya elfu 20 kutoka nje kama tahadhari ya kuwa na akiba katika kipindi hiki cha ugonjwa wa COVID-19.