Alichokisema Waziri kuhusu barakoa za vitambaa
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt Faustine Ndugulile amesema kuwa barakoa za vitambaa hazina ubora wa kinga kama N-95 au zile za upasuaji lakini zinaweza kutumika kupunguza uwezekano wa maambukizi toka kwa mtu mmoja kwenda mwingine.