Mo Dewji na kauli mpya juu ya Simba SC
Mfanyabiashara na muwekezaji wa Klabu ya Simba Mohammed Dewji "Mo", amewatoa wasiwasi wapenzi na mashabiki wa timu hiyo, kwa kusema hakuna mchezaji yeyote atakayeondoka pia watamsajili mchezaji yeyote kutoka popote kama kocha wao akimuhitaji.

