Polisi yaeleza sababu za kumkamata Wakili Msando
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, ACP Koka Moita, amesema kuwa wanamshikilia Wakili wa kujitegemea Albert Msando, baada ya kutoa kauli za uchochezi dhidi ya Serikali juu ya ugonjwa wa COVID-19 kwa madai ya kuwa mkoani humo hali ya maambukizi ni mbaya ili hali yeye hana mamlaka hayo.