Polisi kumsaka Mwalimu aliyemshambulia mwenzake
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro ACP Salum Hamduni, amesema kuwa mara baada ya Mwalimu Agnes Mushi, anayetuhumiwa kumpiga mwanamke mwenzake kwa madai ya kwamba amemfumania na mumewe, kukiuka wito wa jeshi hilo, basi Polisi wataingia wenyewe kumsaka popote alipo na kumkamata.